YAJUE MAKANISA NA MADHEHEBU YALIYOKATALIWA NA MUNGU ALIYE HAI.

[ad_1]


Ndugu msomaji wa makala haya ya Nabii Hebron nakusalimia kwa jina la YESU KRSTO WA  NAZARETI, ukiwa ni mwanadamu aliyekuumba kwa jinsia  ya kike au ya kiume na uwe rangi tofauti na akakupa uhalali wa taifa lolote lile ambalo unaishi sasa, hata hapo unapoishi  ni mali yake yeye ndiye kapaumba.
Utasoma kitabu cha Hosea 4:4-9.

Neno la MUNGU linasema  walakini asishindane mtu , wala mtu asikemee maana watu wako ni kamawao washindanao na kuhani. Na wewe utajikwaa wakati wa mchana, na nabii naye atajikwaa pamoja nawe wakati wa usiku, nami nitamwangamiza mama yako. Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa, kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi, kwa kuwa umeisahau sheria ya MUNGU wako, mimi nami nitawasahau watoto wako. Kadiri walivyozidishwa, kwa kadiri iyo hiyo walinitenda dhambi, nami nitaugeuza utukufu wao kuwa aibu. Hujilisha dhambi ya watu wangu,hujifurahisha moyo kwa uovu wao. Hata itakuwa kama walivyo watu, ndivyo atakavyokuwa kuhani, NAMI NITAWAADHIBU KWA AJILI YA NJIA ZAO, NA KUWALIPA KWA MATENDO YAO.

Ewe mwanadamu katika makala haya ya mtume Hebron, nitakufunulia ukweli halisi ili ujijue upo salama katika kanisa ulilopo au tayari na wewe upo katika kipigo cha MUNGU alichokisema  na baada ya kuujua ukweli uchukue hatua umuombe akuongoze akupeleke katika kanisa analolitaka  yeye.

Ujumbe huu ni kwa ajili ya watu wote katika ulimwengu wote na haya ninayokuandikia katika makala haya , ni maneno halisi yaliyotoka katika kinywa  cha MUNGU aliye hai,aliye viumba viumbe  vyote na pia ndiye BABA yake  YESU KRISTO WA NAZARETI, ambaye ile  siku ya mwisho atakuja  kuuhukumu ulimwengu na kulichukua kanisa ambalo MUNGU AMELIKUBALI na atalihukumu kanisa  ambalo MUNGU amelikataa, na ikiwa na wewe  ni mmoja wapo na upo katika kanisa  hilo alilolikataa MUNGU ujijue na wewe umekataliwa, hivyo funguka ufahamu haya nikuandikiayo ni ili wewe uchukue hatua  na utoke huko usije ukaangamia na umweleze na mwingine utakuwa pia umeifanya kazi ya MUNGU na atakubariki na wewe.

Maana, hii ni siri iliyo fichika katika ulimwengu huu na watu wamepigwa upofu hata wasijijue maana ukijijua tu  tayari umepona wewe siyo mateka wa  wshetani tena.
Kwanzakabisa usome kitabu changu KINACHOITWA JINSI KANISA LILIVYOTEKWA NA SHETANI, utajifunza  mengi zaidi. Katika kitabu cha Hosea 4. MUNGU anasema kwa sababu wamemkataa kuhani mkuu (ambaye ndiye MUNGU mwenyewe), umekataa sheria zake na yeye  amekukataa wewe kuhani unayesimamia  kanisa, na hao waumini wote amewakataa na sababu kubwa ya hata waumini kukataliwa na MUNGU ni sababu  ya kuhani alivyo.


Mchungaji akikubaliwa na MUNGU  na waumini watakubaliwa, ila Akikataliwa na MUNGU na kila kitu akifanyacho kimekataliwa kwa sababu jinsi alivyo kuhani (mtumishi) ndivyo na waumini (kondoo) walivyo na hayo huyaridhi kutoka kwa kuhani
(mchungaji, mwalimu, nabii,mtume,mwinjilisti). Na nitakufundisha ili uelewe namna ya kumtambua kuhani  au kanisa, au dhehebu lililokataliwa na MUNGU  maana kwa macho ya nyama hauwezi kulijua jina lake maana  halijaandikwa katika Biblia ni lipi, ila nitakuelezea ujijue na itabaki akilini, kichwani kwako, maana unayo akili wewe, usiwe tena anayeangamia kwa kukosa maarifa.

Kukosa maarifa ni kutokujua ukweli, na kukosa akili ya kujua jinsi ipasavyo kuwa na ukaenda kinyume, na matokeo yake ni kuangamia. Haijalishi hata kama kuhani analitaja jina la MUNGU na YESU pia, maana unakuta mtu anayetenda kinyume na Neno la MUNGU  huyo ina maana anamtaja kwa mdomo yani nje tu, akitenda sawa sawa na Neno la MUNGU  inamaana MUNGU  yupo ndani ya moyo wake na siyo mnafiki mbele za MUNGU na MUNGU  humpenda kuhani  au hamna lililo linafiki mbele yake na kama ni mnafiki hata maombi yenu na sadaka  mzitoazo  hazipokei na hazitaki.

Mnaibiwa tu na shetani, maana utoapo sadaka lazima uone baraka, uone na mengineyo kuhusu roho yako. (Hosea 8:13-14) kwa habari za dhabihu(sadaka) za matoleo yangu, hutoa dhabihu ya nyama na kuila lakini BWANA hawakubali, sasa ataukumbuka uovu wao, na kuwapatiliza dhambi zao watarudi kwenda Misri. Maana Israeli amemsahau muumba wake, naye amejenga nyumba za enzi, na Yuda ameongeza miji yenye maboma,  lakini nitapeleka moto juu ya miji yake nao utaziteketeza ngome zake.

Ndugu msomaji, umeona mfano halisi ya kuwa kanisa alilolikataa MUNGU hata matoleo yao yaani dhabihu au sadaka hazipokei sababu zina uovu na kama  unatoa ujijue ni sawa  sawa na mtu atupaye chini pesa akaja mtu akaiokota akaenda nayo na wewe bila kupata faida yeyote ile.

Pia lazima ujiulize swali, kwa nini MUNGU alikatae kanisa linaloitwa kwa jina lake naayakubali mengine yanayoitwa  kwa jina lake? Je yeye ni mbaguzi? Jibu ni ; MUNGU husimamia haki yake  na Neno lake tu tena litajwe katika  Roho na kweli ndani ya   kuhani /mtumishi,  akiwa tofauti tu kanisa lote limekataliwa  na MUNGU ila endelelea pia  kusoma vitabu vyangu nilivyoviandika utafunguka zaidi, na utapona hata katika maeneo mengine usiyo yajua wewe, kwa wewe unayetaka  kwenda mbinguni tuu.
Ndani ya vitabu hivyo utaona yakupasayo kufanya ili uende mbinguni.


MAKANISA NA MADHEHEBU YALIYOKATALIWA NA MUNGU NDIYO HAYA UTAYAJUA KWA MATENDO HAYA YAFUATAYO.

a.      Makanisa yote yanayobatiza ubatizo wa kikombe ambao haujatoka kwake yeye aliyeumba mbingu na dunia na hata katika Biblia haupo kabisa na kama haupo ina maana unatokea kwa Mungu asiyejulikana, na hivyo hayo  makanisa ameniambia siyo yake yeye na hajayaanzisha yafanye hayo .

Akaniambia hata hao waanzilishi wa madhehebu hayo siyo yeye aliwatuma wayaanzishe, walitumwa na  mungu asiyejulikana, yaani Roho ya Nabii wa uongo,akanionyesha kuzimu nikawaona wote kwa majina yao na sura zao na wengi wao hata mimi sikuwahi kuwaona  kwa macho yangu tokea kuzaliwa na walishakufa miaka mingi,akaniambia Hebron, hawa ni makuhani wa shetani na sasa ndivyo walivyo na wao  wamerudi kwa baba yao na hao ambao wanaendeleza kazi hiyo ya ubatizo wa kikombe watamfuata baba yao na hata hao wanaoshiriki katika makanisa hayo, akanionyesha upande wa pili nikawaona watumishi waliokufa  ni wengi idadi yao, sikuweza kuwahesabu tena wamevaa yale majoho, yenye misalaba na makofia.
           Wote wapo kuzimu waliokufa, huo ndio ukweli na wote   
           waliobatizwa ubatizo wa  
maji kichwani, isipokuwa watoto wadogo ambao hawajijui.  Akaniambia  karibu  
ninarudi, makao yapo tayari ila watu hakuna idadi kubwa ya kwenda  mbinguni.
Akaniambia hii ndiyo sababu mojawapo, akasema kwa    hasira  nimeyakataa   
Makanisa haya na matoleo yao na waumini wao maana  hawaniabudu mimi  
MUNGU ninayejulikana na Neno langu, mimi niliyemtuma Yohana aje abatize na   
akafanya na hata mwanangu wa peke na yeye alitii , sasa   hawa ni nani hata  wakaidi sheria zangu?

     Mimi  MUNGU ni  wa haki na nitamtendea haki kila mmoja sawa sawa na matendo yake. Akanionyesha upande mwingine nikaona  watumishi wanaojiita wameokoka wanabatiza kwa maji mengi  ila wameongeza hapo jina la mtumishi, halafu  Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, akaniambia  na hawa na makanisa yao na waumini wao wote nimewakataa maana mchungaji huyo ameuchukua utukufu wangu na sikuagiza hivyo hata kwenye Neno langu.(KANISA HILO SILITAKI NA SIPO NALO).

Ujiulize kama MUNGU aliye hai amelikataa na wewe ujijue uliyepo hapo umekataliwa sababu jinsi alivyo nabii ndivyo na kondoo , akiadhibiwa na waumini ndivyo ilivyo.

b.     Makanisa, madhehebu yote yanayoabudu sanamu yote MUNGU aliye hai ameyakataa hata wanaozibusu sanamu makanisani (Hosea 13: 2-3) Neno linasema na sasa wanazidi kufanya dhambi, nao wanajifanyizia sanamu kwa fedha yao, naam, sanamu kwa kadiri ya akili zao, zote pia ni kazi ya mafundi nao huzitaja hivi, wanaume watoao dhabihu na wazibusu ndama.
Kwa sababu hiyo watakuwa  kama wingu la asubuhi, na kama umande utowekao upesi, kama makapi yaliyopeperushwa na tufani sakafuni, na kama moshi utokao katika bomba.

Neno linashuhudia wazi wazi na ukweli mtupu. Mnaacha kumpa MUNGU aliyewaumba busu takatifu, mnavibusu vitu vilivyotengenezwa na kazi ya mafundi (wanadamu), wote na dhehebu au kanisa hilo ameniambia MUNGU hilo amelikataa na wala hawaendi njia ya mbinguni, hao wanaenda njia ya kuzimu wafike alipo mungu asiyejulikana, haijalishi wametumia Biblia au kutaja jina la mwanangu wa pekee na pia wale walioushinda ulimwengu kama Petro, Musa, Maria  na wengineo, hao hawakufanya ujinga  au upumbavu huu .

Waliniabudu kiukweli na kuzifuata sheria zangu  na Neno langu, ndiyo maana wanaketi  katika  mkono wa kuume wa MUNGU BABA, akaniambia alipo yeye wataenda wale tu, wafanyao kama atakavyo yeye na siyo tofauti .
Mimi MUNGU siyo mnafiki na wala siyo kigeugeu.

c.     Makanisa yanayokopa pesa benki na kuwa na mabenki na kufanya biashara na kudai riba. Ameyakataa MUNGU na hayapo katika kitabu chake cha enzi ila yapo katika kitabu cha enzi cha shetani kule kuzimu na yeye ndiye anaye yaongoza katika mipango yote, katika roho na mwili na baadhi yao makuhani  wanajua kabisa hizo biashara hazijatokea mbinguni, maana  mbinguni hakuna mambo ya kudaiana riba na kufilisiana, haya  ni mambo ya  kaisari tu, ya kaisari mpe kaisari  na ya MUNGU mpe MUNGU.

Kanisa liyafanye ya MUNGU tu, peke yake. Ikiwa tofauti tayari kanisa limeachwa na kubaki kama kampuni ya biashara na siyo huduma ya kiroho tena.
Soma  Neno la MUNGU utayaona amekataa pia. Ukifanya aliyoyakataa, tayari na yeye anakukataa na kuwaacha.


NOTE:
99.9 % MAKANISA YOTE YENYE MABENKI DUNIA NZIMA NI WANACHAMA WA FREEMASON NA WAASISI WAO NI WATOA MAKAFARA, NI WACHAWI, WANATUMIA NGUVU ZA GIZA (NA NI WATOTO WA SHETANI).
NDANI YA VIONGOZI IPO ROHO YA SHETANI, NDANI YA MIOYO YAO IMEJIFICHA

d.     WATUMISHI WOTE FREEMASON MEMBER, WAO PAMOJA NA MAKANISA YAO YOTE NA WAUMINI TAYARI WAMEKATALIWA. MUNGU hashirikiani na uchawi (ingia kwenye mtandao google chunguza utayaona majina yaokimwili

e.      Makanisa ya kuchangisha pesa makanisani.

f.       Kutoa huduma kwa kudai pesa kamahospitali ndio umuone mtumishi (huyo tayari ameshakataliwa na MUNGU na ni roho ya shetani ndiyo inayofanya kazi ndani yake na mapepo ya utambuzi wala siyo roho wa MUNGU.

g.     Watumishi wanaojifanyia minada na kuwaambia watu wasaini katika suti au gauni alilolivaa hayo ni mapepo na hao wanaoabudu mahali pa namna hiyo wajue hawapo na MUNGU aliye hai wapo na mungu mfu. Na zaidi  microphone (kipaza sauti) wanazozitumia kuhubiria watumishi hao huwa siyo microphone(kipaza sauti) za  kweli za kibinadamu, huwa ni nyoka ndiyo microphones zao na akimaliza ibada, microphone hiyo, hurudishwa kuzimu  hadi akihubiri.

Ombeni kufunguliwa macho ya rohoni  mtaona live live. Inatisha jamani YESU jina lake linachezewa. Ila ole wao anajua MUNGU atakachofanya. Na wengine wanakueleza nguvu zipo kwenye stika zao, hizo ni hirizi tupu na unapokuwa na stika zao , mafanikio yako na  akili yako huichukua na kuvitumia kipepo na inawekwa kuzimu.

h.     Makanisa yanayoongozwa na watumishi waliojiita au walioitwaga na yeye halafu wakaenda upande wa shetani hao wote wameshakataliwa na ukiwasikiliza hata mahubiri yaounamsikiliza ibilisi tu,  na makanisa  yote yanayopinga wokovu.

i.        Watumishi wanaofanya mazingaumbwe na makanisa yaoyote yamekataliwa na MUNGU (kufufua misukule au kutoa vitu kwenye miili ya wanadamu) wakati wewe unayetolewa hauvioni.(HAO NI WACHAWI) hakuna mtumishi wa MUNGU wa kweli hapo.

j.        Ila mtumishi anayetumia nguvu za gizahukufundisha mistari ya Biblia ya kukufanya wewe umuone ndiye mungu wako, pili  hukusisitiza kuhusu kutoa pesa tu na kukusanya madeni, na kuandika ripoti   za sadaka zako na kukupatia risiti tofauti na Biblia isemavyo asijue mtu yeyote. Na hata ukitoa mahali hapo unatupa tu kamavile chooni. (YAMEKATALIWA)

k.     Makanisa yanayo barikia watoto  wakiwa watu wazima, ni tofauti na alivyoagiza, huo ubarikio hautoki kwake na hao wanaobarikiwa hizo baraka ni za shetani, mtoto YESU alibarikiwa akiwa hajui lolote  huo ndio utoto, hawa wa siku hizi wanajua mpaka uzinzi, walevi, wanajua dhambi ni nini,  Je, hawa ni watoto wadogo? Jibu siyo .

Utasoma katika vitabu vyangu utaelewa maana ya ubarikio, badala ya kuwa baraka ni laana tupu. Mmekataliwa,  na aliyeanzisha ubarikio wa watu wazima amekwisha hukumiwa huyo kuhani, kinachoendelea ni ile roho ya kuasi katika makanisa waliyoyaanzisha chini ya roho ya shetani ili awalaani.

NOTE:

Ndugu msomaji natumaini mpaka hapo umepata picha kidogo au hata sana, na ikiwa unampenda MUNGU na unataka kwenda mbinguni achana na hayo ni bora kama hakuna kanisa unaloona linaenda sawa sawa na Neno la MUNGU ni bora ukae nyumbani tu, na MUNGU atakuona moyo wako kuliko kwenda katika mapango ya wanyang’anyi na kwenda kupokea unajisi au kuwekewa alama ya shetani kwa njia ya roho pasipo wewe kujua, na wewe unampenda YESU ila unapotoshwa na makuhani wenye roho ya shetani ndani ya mioyo yao.

Usomapo  ujumbe huu lazima ndani ya moyo wako utapona ila wapo wale wafanyakazi wa shetani watumishi hao walizoea kusema Nabii walikuwepo zamani za  akina Musa.

Hivyo haya yanayozungumzwa na Nabii Hebron ni porojo au maneno tu?! Mtayaona yote na yatatimia na hakuna wa kuzuia hii ni order  kutoka kwenye kiti cha enzi  alipo  BABA  yangu na alivyonituma  kwa mataifa yote niupeleke ujumbe wake. Na hakuna atakayeweza  kunizuia milele, maana MUNGU hazuiliki ila shetani ndiye anayezuilika na hana uwezo wa kushindana na MUNGU.


NABII HEBRONWILSON KISAMO.

[ad_2]